Kufuatia kifo cha mwanachuo wa chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline, Serikali ya awamu ya tano imepokea bajeti ya milioni 80 ya mazishi na imesema haitatoa pesa hiyo taslimu bali itatoa vitu kwa ajili ya kukamilisha mazishi kama ambavyo iliahidi.

Hivyo kaka wa marehemu, Kiyeyeu ametaja vitu ambavyo serikali imeahidi kuvitoa ambavyo ni jeneza, nguo za marehemu, maua, mashada, magari, kaburi, manukato, kujengea kaburi, chakula, maturubai, viti na muziki ambavyo viliorodheshwa kwenye bajeti iliyotolewa na familia.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,, Leornad Akwilapo amesema wamepokea bajeti hiyo ya milioni 80 na kama serikali haikuipitisha bajeti hiyo kama ilivyo kutokana na baadhi ya mambo ambayo yaliwekwa kwenye kinyume na sheria huku mengine yakiwa kwenye makisio ya gharama za kiwango cha juu.

Aidha Moi Kiyeyeu ambaye ni kaka wa Akwilina amesema walipotoa gharama hiyo ya milioni 80 haikuwa na maana kuishinikiza Serikali itoe fedha hizo bali walilenga fedha hizo zitumike kwa mahitaji ya msiba mpaka pale utakapoisha.

Familia imeishukuru Serikali kwa kuridhia gharama zote za mazishi.

Akwilina Akwiline amefariki dunia Februari 16, 2018 kwa kupigwa risasi ya kichwa alipokuwa kwenye daladala akifanya safari zake, pindi wafuasi wa chadema walipokuwa wakiandamana huku polisi wakijaribu kutuliza ghasia za maandamano hayo.

NEC yatao sababu idadi ndogo ya wapiga kura kinondoni na Siha
Rais wa FIFA atua nchini

Comments

comments