Serikali imepiga marufuku mamlaka zote zilizo chini ya Waziri Mkuu kutoa tamko, kuzungumzia au kufafanua suala la faru John hadi hapo taarifa rasmi ya tume inayochunguza kifo cha mnyama huyo itakapomaliza kazi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani aliwaambia waandishi wa habari jana, ”kwa kuwa suala hili, liliibuliwa na Waziri Mkuu na tayari alitoa maagizo ambayo  baadhi yametekelezwa na wizara ikiwamo kuwasilishwa DVD za kuhamishwa Faru na kuunda tume, hivyo mwenye mamlaka ya kutoa taarifa ni Waziri Mkuu mwenyewe au mwingine ambaye atampa mamlaka.

Baada ya Waziri Mkuu kuibua swal hilo, aliagiza wizara kupeleka taarifa za kitaalamu kuhusiana na mchakato wa kumuhamisha faru John kutoka Creta ya Ngorongoro hadi eneo la Sasakwa Grumet ambapo pembe za mnyama huyo zilipelekwa, ambapo suala lake limekuwa gumzo kubwa nchini hivi sasa.Na uchunguzi wa kubainisha kama kweli pembe hizo ni  za Faru John bado unaendelea.

DC mjema: Wekeni mageti barabarani kudhibiti magari mazito
Makani: Faru John mwachieni Waziri Mkuu