Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba ametaja sababu za kuchelewa kuanza kwa uzalishaji wa Sukari kupitia kiwanda cha Mkulazi ulioanza kutekelezwa mwaka 2017.

Akitaja sababu hizo amesema ni Pamoja na kufuata taratibu sahihi za uzalishaji wa miwa ambapo hutumia zaidi ya miaka mitatu.

Sababu hizo zimebainishwa alipofanya ziara ya kukagua hatua mradi huo ulipofikia na kueleza kuwa awali mradi ulitazamiwa uanze uzalishaji wa sukari mwishoni mwa mwaka 2018/19 na kuchelewa kwasababu za kufuata taratibu za kisasa za uzalishaji wa miwa.

Mradi huo unatekelezwa na serikali kupitia ufadhili wa fedha kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ambao wanaeleza kuwa kufikia sasa wametoa Zaidi ya bilioni 80 kwa ajili ya utekelezaji.

Shah Mjanja: Ligi kuchezwa mkoa mmoja sawa na kucheza ugenini
Bahati Vivier: Kuna jambo la kurekebisha