Serikali nchini, imetoa siku saba kwa maeneo yote yanayofanya uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele na mitetemo kurekebisha changamoto hiyo na kulielekeza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuyafungia maeneo yatakayokaidi maelekezo hayo.

Agizo hilo, limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo hii leo Februari 3, 2023 jijini Dodom na kuongrza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira Sura ya 191, Kifungu cha 106 (5 na 6) kinakataza kupiga kelele kuzidi viwango vilivyoruhusiwa na vilevile ni kosa kupiga kelele kinyume na viwango vilivyoruhusiwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo.

“Kanuni za udhibiti wa kelele na mitetemo za mwaka 2015, zimeainisha viwango vya sauti vinavyoruhusiwa kwenye maeneo ya makazi, biashara, viwanda na hospitali ili kulinda afya ya jamii hivyo, nitoe wito kwa wananchi kutoa taarifa kuhusu kelele na mitetemo kwenye ofisi za serikali za mitaa au ofisi za NEMC,” amesema.

Hatua hiyo, imekuja kutokana na kuongezeka kwa malalamiko ya kelele na mitetemo mwaka 2021/2022 ambapo asilimia 65 ya malalamiko yaliyowasilishwa NEMC yanahusu kelele na mitetemo, hali inayoonesha adhabu za kutozwa faini kwa wanaokamatwa zimezoeleka na hazitoshi.

SJMT na SMZ zinashirikiana kiuchumi: Waziri
Wapinzani wa Young African wamesajili tena