Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikuganya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado halijatoa taarifa rasmi lakini wao wanatoa taadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchi hizi mbili Kenya na Tanzania.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya wanasema kuwa ugonjwa wa Chikunganya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu aina ya Aedes na kusema ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea.

Ambapo ameeleza dalili za ugonjwa huo huambatana na homa kali, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu, kichefuchefu, kizunguzungu na wakati mwingine tumbo kuuma.’

Imeelezwa kuwa dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi siku 7 tangu mtu alipoambukizwa ugonjwa huo kwa kung’atwa na mbu mwenye maambukizi.

Hivyo wananchi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanakwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mapema mara wapatapo dalili za ugonjwa huu ili kuweza kuutambua mapema na kuchukua hatua stahiki.

Umoja wa Afrika wamuita Trump kikaoni, kumuweka ‘kitimoto’
Polisi wawili wafariki Jijini Mbeya