Serikali imetoa wito kwa taasisi za umma  kuzingatia matakwa  ya sheria ya manunuzi kwa kuwasilisha mara moja PPRA,GPN zao za mwaka wa fedha 2016/17 pamoja na matangazo ya  zabuni yaliyopo kwenye zabuni na kwenye GPN hizo kwaajili ya kuchapishwa kwenye TPJ na tovuti ya PPRA.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt.L.Shirima alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa mwitikio mdogo umeendelea kuwepo licha ya juhudi za mamlaka kuzikumbusha kuhusu jukumu lao la kuzingatia sheria  lakini bado wamekuwa wazito.

Aidha bw, Shirima alisema kuwa PPRA imebaini kwamba baadhi ya taasisi zimekuwa zikichapisha GPNs zao kwenye magazeti mengine bila kuwasilisha PPRA,kinyume na sheria ambayo inawataka kuchapisha kwenye jarida la manunuzi na tovuti ya PPRA pekee.

Aliongeza kuwa taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/15 ilibainisha kwamba manunuzi ya shilingi bilioni 8.5 hayakuwa yamejumuishwa kwenye mpango wa manunuzi na kusababisha upotevu wa fedha za umma,uwepo wa vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa sheria ya manunuzi.

Hata  hivyo PPRA ina taarifa za taasisi zote ambazo zilishindwa kuwasilishwa GPNs zao kwa mwaka uliopita wa fedha  wa 2015/16.na inazitaarifu taasisi hizo  kuonyesha ushirikiano na mamlaka nyingine za serikali kuchukua hatua kali dhidi ya maafisa masuuli wa taasisi hizo kwa kushindwa kuchukua kusimamia utekelezaji wa sheria ya manunuzi.

Kanuni ya 70 ya kanuni za manunuzi ya umma za mwaka 2013 inaitaka taasisi nunuzi kuandaa na kuwasilisha PPRA mpango wa manunuzi wa mwaka ndani ya siku 14 baada ya kumalizika kaw mchakato wa bajeti

Video: Meya Wa Manispaa Ya Kinondoni Atumbua Majipu
Video: CHADEMA watoa tamko kufanya mikutano nchi nzima tarehe 1 september 2016