Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi utakaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali  hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Zuma kujibu mashtaka ya rushwa Afrika Kusini
Nyumba zisizo na vyoo bora kutambulishwa kwa bendera nyekundu

Comments

comments