Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa inakadiliwa kwamba wagonjwa wa akili ni asilimia moja tu ya watanzania wote, hivyo kati ya Watanzania milioni 50, wagonjwa wa akili ni watanzania laki 5.

Kati ya hao asilimia 48 wanafika katika vituo vya kutolea huduma za afya, asilimia 24 wanakwenda kwa waganga wa kienyeji na asilimia zilizobaki wanapelekwa katika tiba ya kiroho.

katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma, Serikali imewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhamasisha jamii katika kuwaibua wagonjwa wa akili kuwapeleka katika vituo vya afya ili wapatiwe matibabu bure.

Tamko hilo limetolewa wakati Dk.Ndugulile alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini Prosper Joseph Mbena lihoji kwa nini serikali haina utaratibu wa kuwachukua wagonjwa wa akili wanaorandaranda barabarani na mtaani na kuwapeleka kwenye hospitali za wagonjwa wa akili ili wapatiwe matibabu.

Aidha amesisitiza kuwa sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 inawataka ndugu na jamii wawaibue wagonjwa wa akili na kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma ili wapewe matibabu na wakishapata nafuu waruhusiwe wakae na familia zao.

Kabila kuachia madaraka, ampanga mrithi wake
Marekani yaingilia kati zuio la kufungiwa Televisheni Kenya