Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza watu waliojenga katika maeneo holela kurasimisiwa maeneo hayo ili kuepuka hasara ambayo serikali inaipata kwa kutowatambua.

Akizungumza leo mjini Musoma mkoani Mara katika sehemu ya ziara yake, Waziri Lukuvi alisema kuwa kwa kutowatambua watu hao ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa miaka mingi bila kulipa kodi, serikali inakosa mapato bila sababu za msingi.

“Yule mwananchi aliyejenga katika makazi holela, nyumba ya zamani haumsaidii yeye, anaishi tu. Wewe Halmashauri ya Wilaya ya Musoma unaendelea kumuita yule holela lakini na wewe hupati kodi, kwahiyo wote mnapata hasara,” alisema Waziri Lukuvi.

“Wizara inawaagizeni watu wote waliojenga katika maeneo holela warasimishiwe,” aliongeza.

Waziri Lukuvi yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine, anaangazia migogoro ya ardhi katika maeneo hayo.

Wabunge wa majimbo yanayounda mkoa huo wameonesha ushirikiano wa kwa Waziri Lukuvi katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa changamoto za ardhi.

Melo aachiwa kwa dhamana
Picha 9 za michezo zitakazokuacha mdomo wazi mwaka 2016