Serikali imesema kuwa haitasita kuvifunga viwanda jijini Mwanza vitakavyobainika kuchafua mazingira na kutofuata sheria ya Mazingira.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na Mazingira) Luhaga Mpina alipokuwa akiendelea na ziara yake jijini humo.

Mpina alieleza kuwa viwanda vimebainika kuwa chanzo kikuu cha uchavuzi wa mazingira kwakuwa viwanda vingi hutoa kemikali za sumu kuelekea kwenye mazingira. Hivyo, aliwataka wamiliki wote wa viwanda nchini kuhakikisha wanafanya kila jitihada kudhibiti uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutibu taka za kemikali zinazotoka viwandani humo kabla ya kuzielekeza kwenye mazingira.

“Kwa kawaida, maji yanayotoka viwandani kuelekea kwenye vyanzo vya maji ni lazima yatibiwe na Alkarine. Maji yanayopita kwenye vyanzo vyetu vya maji lazima yawe na PH; 6-8.5,” alisema Mpina.

Alisisitiza kuwa ni bora zaidi nchi ikakosa mapato kutoka kwenye viwanda vinavyochafua mazingira kuliko kuhatarisha afya za wananchi.

Staa wa 'Teen Wolf' ajilipua na hili
Serikali Yakata Rufaa Kupinga kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda