Jamii nchini, imetakiwa kutoa ushirikiano wa utoaji wa taarifa sahihi wanapohitajiwa kufanya hivyo na wataalamu mbalimbali wa masuala ya kimaendeleo, ili waweze kutatuliwa changamoto zinazowakabili kulingana na mahitaji yao.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Siza Tumbo, ameyasema hayo jijini Dodoma leo, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya chakula nchini mwaka 2014/2017, inayowahusisha wadau kutoka Wizarani na Taasisi mbalimbali.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya Wananchi ambao hupotosha taarifa za mahitaji halisi ya shida inalowakabili, wengi wao wakihofia kudaiwa michango au tozo mbalimbali, kitu ambacho huwafanya kukosa stahiki za kimaendeleo kulingana na ukubwa wa tatizo.

Video: Rose Muhando aibuka kwa kumsifia Kenyatta

‘’Mfano mtu unawauliza wafugaji Kijiji chao kina ng’ombe wangapi, lengo ni kujua ukubwa wa bwawa unaloweza kuwachimbia kwa ajili ya kunywesha mifugo, lakini idadi wanayotaja si sahihi, sasa pindi unapowachimbia bwawa linakuwa halitoshelezi mahitaji,’’ amesema Tumbo.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amesema dhamira ya Serikali ni kushirikiana na Wanachama na Wadau katika kuratibu jitihada za mabadiliko ya kisera na mifumo ya utendaji kwa masuala muhimu yanayowaathiri wakulima wadogo.

Daktari awashauri wanaume kulia, ‘msihofie kuchekwa’

Hata hivyo amevisisitiza vyombo vya Habari kuendelea kutoa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya kilimo kwa Wakulima, kitu ambacho kitasaidia kuwafanya wawe na tahadhari au uratibu wa mambo kulingana na ujumbe husika.

‘’Utoaji wa taarifa sahihi sio kwa wakulima pekee, hata vyombo vya habari vinapaswa kuelimisha kwa usahihi, hii itasaidia kufanikisha azma ya takwimu halisi na hatua za kuchukua zilizo stahiki kwa kulingana na ujumbe au taaarifa iliyotolewa,’’ Ameongeza Naibu Katibu Tumbo.

Uzinduzi huo umeratibiwa na Taasisi inayoshughulika na masuala ya kilimo nchini (ANSAF), kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBC), ukiwa na dira ya Jamii ya Kitanzania iliyoondokana na umasikini, inayoongozwa na sera muafaka na utendaji uliotukuka katika sekta ya kilimo yenye mabadiliko ya kiuchumi.

Dalali awapigia chapuo Chilunda, Naddo Azam Fc
Je unatafuta kazi? hapa nafasi mbalimbali za kazi zimetangazwa