Serikali nchini, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa imedhamiria kuwa na mikakati madhubuti katika kukabiliana na maafa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Charles Msangi wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa, na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022.

Mratibu Maafa UNICEF Bi.Judith akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2022.

Amesema, Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati na kikao kazi hicho kiliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Washiriki kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 wakifuatilia kikao hicho.

“Serikali ilifanya Tathmini ya Mahitaji ya Mfumo wa Usimamizi wa Maafa ambapo rasimu ya taarifa ya tathmini ya mahitaji (Needs assessment and proposed system), inahitaji maoni ya wadau ili kuboresha Mfumo utakaopendekezwa wa kusaidia kuimarisha mawasiliano baina ya wadau wa usimamizi wa maafa,” amesema Msangi

Amesema, mfumo huo utatoa tahadhari mapema ili kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kuokoa maisha na mali na kwamba sheria ya Usimamizi wa Maafa kifungu cha 4 imeweka mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano utakaowaunganisha wadau wa masuala ya maafa ili kufuatilia mwenendo wa majanga, hatua za kuzuia na kukabiliana na maafa kwa wakati.

Afisa Sheria Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nelson Hutty akiwasilisha mada kuhusu Sheria yaUsimamizi wa Maafa Na. 6 ya Mwaka 2022 wakati wa kikao hicho Jijini Dodoma.

Idara ya Menejimenti ya Maafa itaendelea kuratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022 huku Mratibu Maafa wa UNICEF, Judith ameeleza kuwa wataendelea kuboresha mashirikiano na wadau ili kuhakikisha wanajenga uwezo kwa wadau wa maafa katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi vijiji.

“UNICEF tupo pamoja na tunaunga mkono jitihada zote zinazofanya na Seikali hivyo tutaendelea kuwajengea uwezo wadau wote na kuwafikia waathirika wa madhara yatokana ya maafa kwa lengo la kupunguza madhara hayo, na kuendelea kuboresha mifumo ya kupashanaji wa habari wakati wa maafa,”amesema Judith.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 8, 2023
Dkt. Tax ateta na Balozi wa Uingereza David Concar