Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuwa na ada elekezi kwa shule binafsi baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wazazi kutokana na ongezeko la ada mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ongezeko la ada katika shule hizo limekuwa likiwaathiri watoto punde wanaporejeshwa nyumbani.

Aidha mbali na suala la ada, naibu waziri huyo pia amezungumzia tabia za baadhi ya shule kuwarudisha watoto nyumbani kwa madai ya kutovuka wastani wa shule wakati kipimo kwa shule za msingi ni mtihani wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili.

”Sasa hapa kuna haja kubwa ya kuweka ada elekezi kwa shule elekezi katika shule hizi za binafsi, sababu hili limekuwa tatizo kubwa hasa kwa watoto ambao wamekuwa wakiathirika kisaikolojia pindi wanapo rudishwa majumbani,”amesema Waitara

Hata hivyo, ameongeza kuwa kulingana na mfumo wa elimu uliopo kwasasa unaendana na mahitaji ya soko inagawa kuna baadhi tu ya vipengele vichache vinavyohitajika kufanyiwa marekebisho, lakini suala la ada kwa shule binafsi linatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka zaidi.

Ado awalipua Bashe na Nape 'Muswada unawahusu hawa'
Democratic wamkalia kooni Trump, asusia kikao