Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu ameonya kuwa Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litachukuliwa hatua kali ikiwa litashindwa kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wasajili wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa kanuni mpya za sheria ya NGOs zinataka Mashirika hayo hapa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Aidha Dkt. Jingu amewataka wasajili hao kuwa misingi ya uwazi na uwajibikaji kama inavyobainishwa katika sheria hiyo imekuja kufuatia haja ya Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Dkt Jingu ameonya pia NGO yoyote itakayobainika kufanya kazi bila kufuata katiba yake itakosa sifa na kupelekea kufutiwa usajili kwa kanuni ya sheria ya NGO ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 inazitaka NGOs kufanya kazi kama ilivyobainishwa katika katiba ya shirika husika.

‘’Kwasasa tayari tumeanza kuzifanyia kazi kimya kimya NGOs zote ambazo zimeshindwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria kwasababu mtu hasipotii sheria sisi tutatumia shuruti na tutashughulika nao kimya kimya.”Amesema Dkt. Jingu.

Hata hivyo, amewataka wasajili hao kusimamia NGOs katika maeneo yao kwa kuzingatia yale yaliyobainishwa katika kanuni za sheria ya NGOs na kuwataka kuwasiliana na Ofisi ya Msajili kila wakati kwa lengo lakupata usaidizi ikiwa kutakuwa na jambo lolote linalowatatiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini. Neema Mwanga amewataka Wasajili Wasaidizi hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria vinginevyo atakayebainika kufumbia maovu ya Mashirika atamuondoa katika nafasi hiyo na kukabidhi jukumu hilo kwa Afisa mwingine hata kama hatakuwa na taaluma ya Maendeleo ya Jamii.

 

Basi la Rungwe Express lapata ajali mbaya mkoani Morogoro
Mertesacker ampigia debe Arsene Wenger