Wizara ya elimu imezieleza shule za Msingi na Sekondari zisizo za Serikali kuwa Wanafunzi wote wapokelewe kwa ajili ya kuendelea na masomo ifikapo Juni 29, 2020.

Burundi: Nkurunziza kuzikwa leo

Imefafaniliwa kuwa, Wanafunzi wanatarajiwa kukamilisha masomo kama ilivyoelekezwa na muhtasari ya madarasa waliyopo, ada za shule zilipwe kulingana na makubaliano yaliyofanyika mwanzoni mwa mwaka wa masomo bila nyongeza yoyote ya ada

Aidha wazazi wametakiwa kuzingatia kuwa kiwango cha ada huwa kinakadiriwa kwa kuzingatia gharama mbalimbali za uendeshaji wa shule, gharama ambazo ziliendelea kuwepo hata muda ambao shule zilikuwa zimefungwa.

Hata hivyo kwa upande wa malipo ya chakula na usafiri, Wizara imeelekeza Kamati/Bodi za shule kufanya uchambuzi wa gharama inayopaswa kupungua kwa siku ambazo Wanafunzi hawakuwa shuleni.

Kocha Tanzania Prisons atangaza vita Jumapili
Young Africans waiwekea kikao Ndanda FC