Serikali imepiga marufuku utoaji wa fedha kwa wakandarasi ambao hawaja onyesha tafiti za uhalisia wa eneo wanalokwenda kufanyia kazi ili kuepuka gharama na hasara na ziada ya fedha zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi husika.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso mara baada ya kukutana na viongozi, wafanyakazi pamoja na wanafunzi wa chuo cha maji nakusema serikali imejiwekea mipango mikubwa ya kumaliza tatizo la maji ikiwa ni pamoja na kusimamia wataalamu wake wanafanya kazi kwa weledi na kutatua tatizo la maji ambalo limekua sugu kwa miaka mingi.

Hata hivyo, Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt. Shija Kazumba ameiomba serikali kuboresha miundombinu wanayoitumia ili kuendana na kasi ya teknolojia ambayo inabadilikia kila kukicha.

 

 

Godbless Lema amshukia mke wa Kafulila
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 23, 2017