Mgombea wa urais wa shirikisho la soka duniani FIFA kutoka barani Afrika, Tokyo Sexwale  amejiondoa kutoka kwenye uchaguzi wa kuchagua mrithi wa Sepp Blatter.

Bw Sexwale, kutoka Afrika Kusini, alitangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho wakati akihutubia kabla ya kura kupigwa, ambapo alisema hataki kugawanya kura na akawahimiza wajumbe waamue kati ya wagombea wanne waliosalia.

Ameahidi kuunga mkono na kufanya kazi na atakayeshinda.

“Nafikisha kampeni yangu kikomo hapa,” amesema.

Wagombea waliosalia ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, na Jerome Champagne.

UEFA Yachezesha Droo Ya 16 Bora Ya Europa League
Tumba Sued ‘Hatihati’ Jumamosi