Katika juhudi za Serikali kupunguza changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba iliyokuwa inazikabili hospitali mbalimbali nchini ambapo hadi sasa imekwishaipatia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sh. bilioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Desemba 1, 2016 wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Manyara aliposimama wilayani Babati akiwa njiani kwenda Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku saba inayotarajiwa kuanza kesho.

Majaliwa amesema suala la dawa kwa sasa linaenda vizuri, hivyo amewataka viongozi wa mikoa kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinavyopelekwa katika hospitali zao zinatumika kama ilivyokusudiwa.

“Suala la dawa linaenda vizuri sasa. Hakikisheni mnadhibiti mianya ya upotevu wa dawa kwenye hospitali zetu kwa kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wa sekta ya afya wasiokuwa waaminifu,” – Majaliwa.

Pia, amewataka viongozi hao kuweka utaratibu wa kujenga hospitali ya rufaa ya mkoa pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuwawezesha kupata huduma ya matibabu bure kwa mwaka mzima.

Aidha, Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wanakwenda shule ifikapo Januari, ambapo amewataka Maofisa Elimu kushirikiana na halmashauri kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa kwaasilimia 100.

Majaliwa amezungumzia pia kuhusu suala la utoro na mimba kwa watoto wa kike, amewataka viongozi hao kudhibiti jambo hilo kwa kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi wa wanafunzi hao.

Video: 'Hali ya mazingira nchini ni tete' - Makamba
Mapya Yaibuka Kuhusu Langa Lesse Bercy, TFF yanena kuhusu tetesi za kifo chake