Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC Shaban Idd Chilunda, amekamilisha usajili wa kujiunga na CD Tenerefe inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispainia.

Mshambuliaji huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Tenerefe anakuwa mchezaji wa pili kutokea Azam Fc kujiunga na timu hiyo baada ya Farid Mussa ambaye anaichezea timu hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.

Aidha, imeelezwa kuwa Chilunda anatarajia kuungana na timu hiyo muda wowote kutaka hivi sasa pindi vibali vya kufanya kazi nchini Hispania vitakapo kamilia.

Chilunda aliibuka mfungaji bora wa kikosi cha Azam kwenye msimu ligi  uliomalizika baada ya kufunga magoli 10, huku akiwa na mabao matatu kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup inayoendelea jijini Dar Es Salaam.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 7, 2018
Waziri wa zamani wa Pakistan ahukumiwa miaka 10 jela

Comments

comments