Mfalme Kiba kama anavyojiita, leo amejikuta kwenye mtego wa shabiki aliyemuuliza swali jepesi ambalo huenda lingempelekea kutengeneza habari kubwa ya siku ambayo bila shaka ingewapa points nyingi timu hasimu kwake.

Kiba alikutana na swali hilo la shabiki akiwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV ambapo mtangazaji Sam Misago alilisoma kwa ‘mbwembwe’ swali lililoulizwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

“Kuna mtu anauliza hapa Facebook, ‘muulize Ali Kiba, ni mnyama gani wa porini ambaye anamuogopa zaidi ya wanyama wote?’,” Sam alieleza.

Kwa kawaida, swali hili ni la kawaida kabisa. Lakini kwa jicho la tatu ulikuwa mtego wa aina yake ambao bila shaka Ali Kiba aliushtukia kutokana na namna alivyotoa majibu.

Kwa haraka haraka, mnyama anayeogopwa zaidi porini na watu wengi zaidi ni ‘Simba’ ambaye ni mnyama anayetajwa kuwa mfalme wa pori.

Kwanini ni mtego? Mwishoni mwa mwaka uliopita, Diamond Platinumz ambaye kimuziki anatajwa kuwa mpinzani mkubwa wa Ali Kiba, alijibatiza jina la ‘Simba’.

Bila shaka umeuona mtego uliokuwepo kwa Ali Kiba.

Hata hivyo, Ali Kiba ambaye ni Balozi wa Wild Aid inayoendesha kampeni ya kupinga ujangili dhidi ya Tembo, aligoma kumtaja mnyama mmoja.

“wapo wanyama wengi ninaowaogopa porini, mnyama yeyote anayedhuru lazima nimuogope, ambao hawadhuru siwaogopi,” alijibu.

Sekunde chache baadae, alionesha kuushtukia mchezo wa swali hilo zaidi na kujikuta akisema, “wewe… wewe vipi jamaa… wewe jamaa vipi…”

Zitto ampa hili Magufuli... ashindilia msumari wanaokwepa mali, madeni yao kuonekana
Habari Mpasuko: Infantino awa Rais mpya wa FIFA