Mchambuzi Nguli wa Habari za Michezo nchini Tanzania Shaffih Dauda Ameunga mkono hoja za Afisa Mtendaji Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Barbara Gonzalez kuhusu klabu hiyo kukataa kuvaa nembo ya mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22 kampuni ya GSM.

Shirikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’ ilisaini mkataba wa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 na kampuni ya GSM, ambayo inatambulika kama Mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Shaffih Dauda ameandika kwenye Ukurasa wake wa Instagram : “Ni suala tu la (TFF) kutuambia wametumia kanuni ipi kwenye hayo makubaliano yao, Kanuni ya (16) ya udhamini inasema, Nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu itawekwa kwa rangi zake halisi katika mkono wa kulia kwenye sare (Jezi) za timu za kuchezea, na timu zitalazimika kufanya hivyo kwa michezo yote”

“Haya (TFF) mtuambie mmetumia kanuni ipi ? Ligi inawadhamini wakuu wangapi ? (GSM) wakae kushoto kwa kanuni ipi ? Huu msiba umefana sana, hakuna mtu anapaswa kulia nje ya key.”

“BODI, BODI, IWE HURU”
“Free body ya ligi”
Shaffih Dauda Mchambuzi

RC Makalla: Tumeanza kampeni ya kupendezesha Dar es salaam
Mayele atamba kuifunga Simba SC Jumamosi