Shahidi wa tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu ameanza kutoa ushahidi wake leo septemba 20, 2021 katika Mahakama ya Kuu ya Tanzania Division ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Shahidi yhuyo kutoka kituo cha Polisi Osterbay mwenye namba H 4323 Constable Msemwa ambaye ameongozwa kutoa ushahidi ushahidi wake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele ye Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza shauri hilo.

Msemwa ametoa ushahidi wake, baada ya shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo, Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Mahita Mahita kumaliza kutoa ushahidi wake na kisha kuhojiwa na mawakili wa upande wa utetezi kuhusiana na ushahidi alioutoa mahakamani hapo, kuhusiana na kielelezo kinachobishaniwa na upande wa utetezi.

Itakumbukwa kesi ya Mbowe na mwenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.

Jaji Mutungi kukutana na vyombo vya ulinzi na usalama
Rais wa Zambia asafiri kwa ndege ya abiria