Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeelezwa kuwa washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 17 kila mmoja ili kuweza kutimiza adhma hiyo.

Hayo yamesemwa katika maelezo ya mshtakiwa wa saba katika kesi hiyo, Ally Mussa Majeshi yaliyosomwa mahakamani hapo na shahidi wa 10  wa upande wa mashtaka, Sajini Atway Omary baada ya kupokelewa kama kielelezo.

Aidha, Jopo la utetezi linaloundwa na mawakili, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu wamepinga maelezo hayo huku wakisema mshtakiwa alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na polisi.

Hata hivyo, bilionea Msuya aliyekuwa akimiliki vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya Arusha aliuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, 2013 maeneo ya Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

 

Video: Nitashangaa kama wakikosa mikopo- JPM
LIVE IKULU: Rais Magufuli akiwaapisha makatibu wakuu, naibu makatibu na wakuu wa mikoa