Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umewataka watendaji na watumishi wa Makao Makuu ya jumuiya hiyo  kuanza kujipima, kujitathmini na kujipanga upya kimkakati  kwa sababu muda wa  kupiga maneno haupo ila  vinavyohitajika ni uwezo binafsi  na vitendo.
Hayo  yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu  UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka amesema hayoa alipokutana na  kufanya kikao na watumishi wa UVCCM  Makao Makuu  kwa ajili ya kutathmini utendaji wa jumuiya kwa mwaka 2016 na kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu kwa mwaka  2017.
Shaka amesema  kuwa pamoja na kusikiliza michango , maoni , ushauri , mawazo na changamoto zinazowakabili watumishi na namna ya kuzitatua kwa mwaka 2017  lazima uwe mwaka  wa vitendo na mafanikio.
“Tutabadili kila kona yenye kasoro au dosari , lengo si kukomoana ila ni katika kujipanga tena upya, asiyeweza aseme hawezi ili akae kando , kama mtu  hajimudu hatapewa dhamana yoyote kwasababu ya ushikaji na urafiki “Amesema Shaka.
Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema makao makuu inahitaji kuwa kama kioo, sifa ya kioo ni kujiona na kujitambua, kama umechafuka jisafishe ili uwe nadhifu na makini bila mtu  kusukumwa.
Hata hivyo Shaka  amewataka wana  jumuiya mahali popote  walipo nchini wajione  na kujihesabu wao ni ndugu wa tumbo moja, wapendane, wasikubali kukaribisha majungu au hasama kwasababu zama hizo zimepita na hazitarejea tena.

Waziri Mkuu azindua mradi wa maji kata ya Mkongotema
Tume ya mipango wakagua ujenzi wa barabara za juu (flyovers)