Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewataka wanachama, Viongozi, Wabunge na Madiwani  wanao hisi kunyanayasika ndani ya CCM, hawana haja ya kuendelea kuwa wanachama wa chama hicho.

Hayo yamesemwa na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa Umoja huo kata ya Emboret wilaya ya Simanjiro.

Shaka alisema kuna baadhi ya wanachama wanazungumza siri za chama kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kukipaka matope chama hicho kwa visingizio ambavyo sio vya kweli na havina msingi wowote.

“Anayejihisi kubaki kwake ndani ya CCM ana nyanyasika au anapata bughudha, atimke zake aende kokote  anakotaka ila ajue kuwa chama hakitatikisika”alisema Shaka.

Hata hivyo Shaka amewataka vijana wenye sifa, uzalendo, ukereketwa na nidhamu kujiandaa na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali  za uongozi katika umoja huo.

Makonda awataka wazazi kutoa malezi bora kwa watoto
Rais Malinzi Akumbuka Ukarimu Wa Shekiondo