Wanakijiji wasiopungua 15, wameuawa na watu wasiojulikana baada ya kutokea kwa uvamizi wa eneo la Irumu lililopo Jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jirani na mpaka wa nchi ya Uganda.

Shambulizi hilo jipya, linahisiwa kutekelezwa na moja ya makundi yenye silaha ambayo ambayo yamefanya uharibifu mkubwa na kumwaga damu katika eneo hilo la Allied Democratic Forces, ADF.

Mauaji hayo yaliwaathiri zaidi Wanawake na mtoto wa takriban miaka miwili ambapo inasadikika watu watu hao wenye silaha walilenga vijiji vitatu kwa wakati mmoja, kabla ya jeshi kuingilia kati na kutuliza hali hiyo.

ADF, inadaiwa kuendeleza uhalifu tangu mwanzoni mwa mwaka 2023 katika eneo la Beni, mkoa jirani wa Kivu Kaskazini huku wakidaiwa kuhusika na mauaji ya watu 23 huko Makugwe, na kushambulia kanisa moja huko Kasindi, ambalo liliua takriban watu 14.

Khalid Aucho amuibua Nasreddine Nabi
Fenabahce kumpiga bei Samatta, Al Ahly yakomaa