Shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani nchini Afghanistan limemuua Kiongozi Mkuu wa Al Qaeda na mpangaji Mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001 Ayman al-Zawahri (71).

Zawahri, Alitwaa uongozi wa Al Qaeda baada ya vikosi vya Marekani kumuua Osama bin Laden mwaka 2011 ambapo Rais wa Marekani, Joe Biden katika hotuba yake kwa Wananchi wake amesema, “Haki imetolewa, na kiongozi huyu wa kigaidi hayupo tena.”

Shambulio hilo la katikati mwa jiji la Kabul mwishoni mwa juma, lilikuwa ni la kwanza la Marekani nchini Afghanistan, tangu majeshi yake kuondoka nchini humo mwaka 2021 na tayari kundi la Taliban limelaani operesheni hiyo.

Zawahri, alizaliwa Misri na kupata mafunzo kama daktari wa upasuaji kabla ya kuwa mwanajihadi na alitengeneza kikamilifu kundi la Al Qaeda na harakati zake za kigaidi kwa maandishi na hoja zake. huku akitegemewa kwa kiasi kikubwa na shirika lakini kifo chake kinaweza kuwa na athari ndogo kwa shughuli zao za kila.

Kifo choa Kiongozi huyo, ni ushindi muhimu kwa Serikali ya Biden za kukabiliana na ugaidi, na hivyo kuimarisha hoja ya Rais kwamba Marekani bado inaweza kupambana na mashirika ya kigaidi bila kutuma vikosi vya ardhini.

Hata hivyo, Marekani inadai kwamba Taliban ilikiuka makubaliano ya amani kwa kuruhusu al-Zawahri kuingia Afghanistan huku Kundi la Taliban likidai kuwa Marekani ndiyo ilikiuka makubaliano ya amani kwa kufanya shambulio hilo.

Waziri Aweso atoa bei elekezi ya maji
Dkt. Mpango atoa maagizo kwa Wizara za uwekezaji na Fedha