Kufuatia kitendo cha mwanadada Mange Kimambi kumuandika mitandaoni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada huyo na kumwambia kuwa huu ni mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi au mikono yake kudhalilisha watu.

Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa.

Mange Kimambi kupitia ukurasa wake wa instagram amesambaza picha ya kiongozi huyo na kusema kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kuisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi ulimpa mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya” Al Haji Mussa Salimu .

Hata hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya kutomjibu Mange Kimambi  na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe sana lakini amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa ulimi wake na mikono yake.

Aliyehusika mauaji ya Radio atiwa mbaroni
Epuka yafuatayo kujikinga na saratani

Comments

comments