Baraza la Ulamaa likiongozwa na Mwenyekiti wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum wa Mkoa wa Dar es salaam kuanzia Februari 02, 2023.

Uamuzi huo, umefikiwa baada ya kufanyika kwa kikao chake Jumatano February 1-2, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Alhad Mussa Salum

Kufuatia utenguzi huo, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally amemteua Sheikh Walid Alhad Omar, kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dares Salaam kuanzia February 02, 2023.

CCM Kagera wakagua miradi ya maendeleo, wapanda miti
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 3, 2023