Katibu Mkuu wa Jumuiya ya  mashirika ya kiislamu nchini Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa maeneo maalum mjini Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.

Ambapo Ponda alipewa muda wa masaa 72 kuanzia jana kujisalimisha kabla hajatafutwa na polisi.

Kiongozi huyo wa dini aliwasili katika kituo hicho cha polisi siku ya Ijumaa akiwa na wakili wake Abdallah Safari.

Ambapo RPC Mambosasa siku ya Alhamisi alimtaka Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi kwa kuikejeli serikali pindi akizungumza na vyombo vya habari.

Kulingana na kamanda huyo, Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini

Na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo iliamriwa akamatwe na polisi.

 

Serikali yasitisha mnada wa Tanzanite
Polisi kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa makundi whatsApp, kudhibiti uhalifu