Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, imeeleza kuwa waumini hao wamekwama Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere tangu Agosti 23, baada ya taasisi hiyo kuchukua hadi shilingi milioni 10 kutoka kwa kila hujaji, lakini ikashindwa kufanikisha safari hiyo.

“Zipo taasisi zenye tabia ya kuwatapeli waumini na hii si mara ya kwanza. Niwape faraja mahujaji waliokwama kwamba kama mwaka huu hawajasafiri labda Mwenyezi Mungu alipanga wasafiri mwaka ujao. Cha msingi ni kuwa makini na kampuni za aina hii,” amesema.

“Kuna waumini wengine wamezuiwa kuingia Saudi Arabia kwa sababu taasisi zilizowasafirisha nazo hazina vibali vya kuingia huko. Sasa ni kwa nini wasafirishe watu wakati wanajua wazi kwamba hawajatimiza vigezo?”

Aidha, kwa upande wa waumini waliokwama kusafiri wameiomba Serikali kuingilia kati ili warejeshewe fedha zao, kwani hadi sasa hawana matumaini ya kusafiri tena. “Hakuna matumaini tena kama taasisi hii inaweza kutusafirisha, maana tangu Agosti 23 tumeganda hapa na hatujui tufanye nini,” amesema muumini mmoja.

Lema apigwa marufuku kufanya mkutano
Zitto ang'ata na kupuliza Serikalini