Ni maajabu, kichekesho au tukio la kusikitisha kwa nchi zetu zilizostaarabika ambapo juhudi za kudumisha utamaduni wetu zimekuwa zikirudishwa nyuma na utandawazi. Hili nalo ni tukio kichaa lakini limepewa siku maalum!

Maelfu ya watu, wake kwa waume kutoka katika nchi takribani 25 duniani kote, jana walionekana wakiwa katika mitaa mbalimbali ya majiji yao wakiwa wamevaa nguo za ndani (chup*) kwa lengo la kuadhimisha siku ya kutojistili (No Pants Day).

No Pants3

Washerehekeaji walionekana wakiwa katikati ya majiji ya New York, Tokyo, Madrid hadi Moscow wakiwa wanatembelea sehemu zenye mikusanyiko na vituo vya treni za abiria wakiwa katika hali hiyo.

No Pants2

Masharti ya kushiriki sherehe hizo yalikuwa, moja kuwa tayari kuondoa suruali/sketi yako na kubaki na nguo ya ndani katikati ya umati. Pili, Kutoona haya kuhusu suala hilo.

No Pants4

“Kaa ndani ya gari kama ambavyo ungeweza kukaa ukiwa kawaida. Soma jarida au chochote ambacho ungependa kufanya kwa kawaida. Kiongozi wenu atakuwa tayari kuwagawanya katika makundi madogomadogo, na kuwapangia vituo maalum ambapo mtavua,” yalieleza masharti ya washiriki wa sherehe hizo yaliyowekwa kwenye mitandao.

Sherehe hizo ziliratibiwa na Improv Everywhere na zilianzia New York mwaka 2002.

 

'Zanzibar Majipu Yapo'
Picha: Jay Z na Beyonce walivyosherehekea ‘Birthday’ ya Binti yao