Serikali ya Zambia imefanya marekebisho kwenye sheria ya kazi ili kutoa likizo ya siku moja kila mwezi kwa wanawake wawapo kwenye hedhi.

Siku hiyo imepewa jina la ‘Siku ya Mama’, ingawa inawahusu wanawake wote bila kujali kama wana watoto au la.

Kutokana na tasfiri ya kisheria ya kifungu hicho, mwanamke yoyote anayefanya kazi atakuwa na nafasi ya kupumzika siku moja ya kazi kila mwezi bila kujali ni siku gani na kwamba hapaswi kuwasilisha vielelezo vyovyote vya kitabibu.

Kadhalika, wanawake wa Zambia hawapaswi kufanya utaratibu wowote wa kiofisi katika siku hiyo bali wanaweza kubaki nyumbani na kupiga simu kwa waajiriwa wao kuwaeleza kuwa wana mapumziko ya ‘Siku ya Mama’.

Muajiri atakayemzuia mwanamke yoyote kuchukua mapumziko hayo atakuwa katika hatari ya kushitakiwa na kupigwa adhabu kali ya kisheria.

Wanawake nchini humo wameeleza kufurahishwa na sheria hiyo wakidai kuwa siku hiyo moja inawasaidia kupumzika wakati wakiwa kwenye siku zao kwani hupitia mengi.

“Nadhani ni sheria nzuri kwa sababu wanawake tunapitia mengi tunapokuwa kwenye siku za hedhi,” Ndekela Mazimba, mtaalam wa mahusiano ya umma anakaririwa.

Wengine walieleza kuwa siku hiyo ni muhimu kwani hutumika kupumzika na kusaidia kukabiliana na maumizi ya tumbo ya siku moja angalau kwa wale wanaokumbwa na athari za maumivu hayo.

Hata hivyo, ni mwiko (kitamaduni) nchini Zambia kujadili masuala ya hedhi ya wanawake hadharani.

Dhamana ya Lema yatua Mahakama ya Rufaa
Mkuu wa tume ya uchaguzi Gambia akimbilia mafichoni