Nchini Indonesia, Bunge limepitisha sheria iliyofanyiwa mageuzi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na ikivitazama vitendo vya zinaa kwa raia na wageni wanaoitembelea nchi hiyo kuwa ni kosa la jinai inayoweza kumfunga mtu jela hadi mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Sheria na Haki zaBinadamu nchini humo, Edward Hiariej amesema sheria hiyo mpya yenye utata, sasa inapaswa kusainiwa na rais ili iwe sheria kamili.

Ukumbi wa Bunge nchini Indonesia. Picha ya Vietnamplus.

Naibu waziri huyo amesema, sheria hiyo haitotekelezwa mara moja na inaweza kuchukua mpaka miaka mitatu kuondokana na sheria ya zamani ili kuweza kuitekeleza sheria mpya.

Aidha, kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanywa, mtu anaweza kukabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kushiriki ngono nje ya ndoa ingawa mashitaka yanayohusu zinaa yanapaswa kuzingatia ripoti za Polisi zilizowasilishwa na wanandoa, mzazi au mtoto.

Polisi yateta na jamii mapambano ukatili kwa Wanawake na Watoto
Young Africans yawasili Ruangwa kwa kishindo