Serikali imependekeza mfumo wa ufuatiliaji na tathmini wa uboreshaji nidhamu ya utendaji kazi katika idara mbalimbali uwepo kisheria ili uweze kutekelezwa kwa taasisi zote za umma nchini.

Pendekezo hilo limetolewa na Naibu Katibu mkuu ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Francis Michael Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa ufuatiliaji na tathmini ya watendaji wa Serikali.

Dkt. Michael ambaye alikua akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma Dkt. Laurean Ndumbaro amesema matumizi sahihi ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini Serikalini yataongeza uwajibikaji na kuboresha utendaji wa kazi.

Kigwangalla amtetea Idris kwa ku-edit picha ya Rais, Makonda ‘jisalimishe polisi’

“Mfumo huu ukikaa kisheria utaongeza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma nchini na hivyo kuwa na mchango katika maendeleo ya utumishi na taifa kwa ujumla kwa kuwa na mfumo sahihi wa ufuatiliaji wa tathmini ili kuboresha nidhamu,” amefafanua Dkt. Michael.

Amesema pamoja na kuanzisha sehemu za ufuatiliaji na tathmini kwenye Wizara, idara zinazojitegemea, sekretarieti za Mikoa na mamlaka za serikali za mitaa pia ni muhimu kwa viongozi wenye dhamana kuwa na utashi wa kisiasa katika kujenga mfumo huo kitaifa.

Dkt. Michael ameongeza kuwa mfumo huo pia unatakiwa kumgusa mtumishi mmoja mmoja na taasisi kwa ujumla na kwamba kwa kufanikisha jambo hilo watakuwa hawana budi kuonesha matokeo chanya kulingana na rasilimali zilizopo.

Hofu yatanda Mtwara, Watoto 11 watoweka

“Watumishi na taasisi watakuwa hawana budi kuonyesha matokeo chanya kwa kutumia rasilimali zilizopo na kwa upande mwingine
wananchi wana haki ya kuiwajibisha Serikali kwa kuitaka ionyeshe matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,” amebainisha Naibu Katibimu huyo.

Awali Mkurugenzi wa centre for learning on evaluation and results (CLEAR-AA) kutoka chuo cha Witwatersrand nchini Afrika ya kusini Prof. Dugan Fraser amesema wapo tayari kushirikiana na Serikali katika kuwezesha matumizi sahihi ya mfumo huo.

Amesema amesikitishwa na baadhi ya watendaji wanaotumia muda mwingi kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali na kutoa taarifa za miradi hiyo kwa kuchelewa.

Kero za mabango kwa Waziri Mkuu zaanza kusikilizwa

“Kitendo kama hiki kinasababisha taarifa zilizopatikana kutokuwa na mchango chanya
katika kufanya maamuzi maana wafuatiliaji wanakuwa wanatumia muda mrefu kufanikisha ufuatiliaji hivyo ni wazi mabadiliko yanahitajika,” amefafanua Prof. Fraser.

Hata hivyo Prof. Fraser amebainisha kuwa nchi isiyotumia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini katika utekelezaji wa miradi yake husababisha kuwa na sera mbovu, wananchi kutopata haki ya kuishauri serikali au kutoa maoni juu ya utekelezaji wa miradi, na serikali husika kutekeleza programu za maendeleo bila ufanisi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa idara ya uchambuzi na ushauri wa kazi, ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Nolasco Kipanda amesema kufanyika kwa semina hiyo kunatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali za kuwajengea uwezo
kiutendaji wataalamu wake wa ufuatiliaji na tathmini.

“Kutokana na jitihada hizi za Serikali ninawataka wataalamu husika kutumia fursa hii kuongeza ujuzi ili wawe na tija kwa maendeleo ya taifa,” ameongeza Kipanda.

Semina hiyo imehudhuriwa na wadau kutoka Wizarani, idara zinazojitegemea, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa, Mahakama, Bunge, Tanzania Evaluation Association (TanEA) na washirika kutoka Afrika Kusini ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ufuatiliaji na tathmini.

 

NI VITA: Ali Kiba amporomoshea mawe Diamond, ‘UNIKOME... au nikuweke uchi’
Kigwangalla amtetea Idris kwa ku-edit picha ya Rais, Makonda ‘jisalimishe polisi’