Klabu za soka nchini England, zitaruhusiwa kutumia wachezaji wa akiba wanne wakati wa Dakika za nyongeza 30, kwenye hatua za mwisho za michuano ya kombe la FA (FA Cup) katika msimu wa 2016/07.

Sheria hii mpya itatumika kuanzia robo fainali za FA Cup.

Uamuzi huu unaenda sambamba na mabadiliko ya kufuta michezo ya marudiano endapo timu zitaenda Sare kuanzia Robo fainali.

Michuano ya FA Cup ipangwa kuanza Agosti 5 kwa Michezo 184 ya mzunguuko wa kwanza ambao hautazishirikisha klabu za ligi kuu England na ligi daraja la kwanza Championship.

Wakati huo huo chombo chenye mamlaka ya kubadili Sheria za Soka (IFAB-International Football Association), kinatarajia kubariki sheria ya kuwatumia wachezaji wanne wa akiba katika michuano yote iliyo chini ya FIFA.

Mfumo huu wa kutumia wachezaji wane wa akiba badala ya Watatu, ulijaribiwa kwenye michuano ya Copa America ya mwaka 2016, iliyofanyika nchini Marekani.

Ni Marufuku Kwa Wachezaji Wa Man City Kula Pizza
CHADEMA watangaza Mikutano, Maandamano Nchi Nzima