Klabu ya Cs Constantine inayoshiriki Ligi kuu nchini Algeria imemsajili aliyekua kiungo wa mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, Sharaf Shiboub kwa mkataba wa miaka miwili.

Shiboub aliachwa na Simba SC, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita, huku sababu nyingine iliyomkosesha dili la kuendelea kukipiga Msimbazi ni kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania Bara mara tatu mfululizo.

Kampuni ya uwakala ya Sifezasports inayofanya kazi na kiungo huyo kutoka nchini Sudan, imethibitisha katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa, Shiboub amejiunga na klabu ya Cs Constantine.

“Mteja wetu amekubaliana kujiunga Cs Constatine na hii ni klabu kubwa yenye mtaji wa mashabiki katika Ligi ya Algeria”.

Shiboub na Simba SC kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea katika klabu ya Al Hillal ya nyumbani kwao Sudan.

Manchester Utd warudisha majeshi kwa Sancho
Serikali ya CCM kuboresha huduma za afya