Msanii Nuh Mziwanda ameachia video ya wimbo wake ‘Jike Shupa’ akiwa amemshirikisha Ali Kiba. Ex wa Nuh Mziwanda ambaye ni msanii Shilole ameonyesha kukasirishwa na baadhi ya maigizo yaliyoonyeshwa kwenye video hio.

Katika Video hiyo kuna mwanamke anayedaiwa kufanana na Shilole akifanya matendo ambaye awali Shishi aliyafanya kwa Nuh Mziwanda kama kupigana na kumpokonya simu.

Shilole ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu video hiyo ya Nuh Mziwanda.

“…Umemiss mkong’oto?? Sipendagi mwanaume mjinga ndo maana umekula mikongoto yakutosha…” – Shilole       Dongo

Hii hapa video ya Nuh na Ali Kiba ‘Jike Shupa’ unaweza kuitazama kisha acha comments zako zitamfikia Nuh Mziwanda 

Everton Wamalizana Na Ronald Koeman
Yasemavyo Magazeti Ya Leo Kuhusu Usajili Wa Barani Ulaya