Msanii wa Muziki Bongo na mjasiliamali ambaye amewahi kuingia katika bifu na msanii mwenza Snura, Zuwena maarufu kama Shishi Trump au Shilole ameweka wazi juu ya suala la utimu na kusema kuwa yeye ni timu Diamond na si timu Alikiba.

Shishi amesema kuwa Diamond ni kaka yake na anauwezo wa kumipigia simu muda wowote na shida yake ikatatuliwa mara moja.

”Mimi ni Timu Diamond Platinum, Diamond ni kaka yangu sababu anasapoti wasanii wengine, unajua kuna msanii tunakuwa na faida naye lakini kuna msanii yupo lakini hatuna faida naye, Diamond anafaida na watu wengi sana wengi anawasapoti kwenye muziki wengi anawaspoti kwenye maisha ya kawaida” amesema Shilole.

Aidha amezungumzia juu ya nyumba aliyoipost mtandaoni ambayo ipo mbioni kumalizika katika harakati za ujenzi amesema kuwa nyumba hiyo ameijenga maalumu kwa ajili ya watoto na kuishi na mume wake Uchebe.

Ameongezea kuwa nyumba hiyo ameijenga kwa muda wa miaka mitatu huku akiwa anadunduliza pesa ili kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa moja kati ya mama wenye nyumba hapa mjini.

Shilole amezungumza hayo mapema leo hii pindi alipofanya mahojiano na chombo cha habari mtandaoni cha Dizzim.

Askari waliowapiga wanahabari kutiwa mbaroni
Wakulima 17 wanufaika na MKURABITA