Ulimi wa shilole umetoa nafasi moja ya ajira kwa Mtanzani atakayeweza kumfunza lugha ya Kiingereza hadi ulimi wake ukidhi vigezo vya kuongea na rapa wa Young Money, Nicki Minaj ambaye amedai atakutana naye hivi punde!

Msanii huyo kutoka Igunga amekuwa akiwavunja mbavu wajuzi wa lugha za kigeni mara kadhaa anapoamua kuzungumza au kuandika kiingereza hususan alipokuwa na mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda.

Msanii huyo ameweka kwenye Instagram namba ya simu itakayomuwezesha mtu anayeitaka kazi hiyo kufanikiwa kumfikia haraka. Kazi kwako.

“TANGAZO MUHIMU. Anatafutwa mwalimu wa kiingerezaaa mzuriii. Jamani huu sio utani nipo sirias naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa Na Nikiminaji hivyo lazima nijinoeee namba ya sm 0653883839 #saymaname” ameandika.

AY afunguka baada ya TCRA kuifungia video ya ‘Zigo Remix’, TCRA nao wanena
Habari Mpasuko: Mahakama yatupilia mbali kesi ya Kupinga Ubunge wa Msigwa