Muigizaji na muimbaji, Shilole ametoa ‘mahubiri’ yake kwa vijana wenzake wanaoyatamani mafanikio akiwataka wamtangulize Mungu kwa kila jambo.

Shilole amewataka vijana watafutaji hasa wasichana kutokatishwa tamaa na changamoto mbalimbali zinazowakabili bali waige mfano wake wa kuyapitia magumu na kutomtumaini Binadamu ila Mungu pekee.

“Nilikotoka ni mbali sana ni Mungu ndiye anajua,hivyo usikubali kukatishwa taaa na binadamu, Coz huwezi jua ridhiki yako ipo wapi (sometimes) huwa mnaona kama nawachekesha ila mnapaswa mjifunze kupitia mimi hasa akinadada, mazuri yangu chukueni mabaya yangu yaacheni!Jifunzeni kujituma na kutokata tamaa mimi ningekata tamaa nisingefika hapa nilipo na tumtangulize Mungu mbele.” alisema Shilole.

Chanzo: Times Fm

Neymar Aanza Kuzigombanisha Man Utd, Man City
Laurent Koscielny: Ninajihisi Faraja Kuwa Nahodha Wa Arsenal