Mjasiliamali na msanii wa muziki wa bongo Fleva maarufu kama Shilole amepinga vikali na kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Muna Love ambaye ni mama mzazi wa marehemu Patrick aliyefariki dunia siku chache zilizopita kuita vyombo vya habari kuongelea habari za baba wa mtoto na juu ya kifo cha mtoto wake Patrick.

Amesema kuwa Muna hakuwa na haja ya kufanya hivyo kwani hata 40 ya mtoto wake bado haijafika alitakiwa kukaa kimya na kuacha mambo yapite kama alivyofanya Casto na Peter,

”Alichokifanya Muna ni kudhalilisha wanawake wenzie waonekane hawana moyo” Amesema Shilole.

Shilole kupitia ukurasa wa Instgram ameandika ” Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho ngumu kwenye hii dunia kama Muna”.

Shilole amesema kama alikuwa na tatizo angemtafuta ili amshauri na sio kuita vyombo vya habari kuzungumza vitu ambavyo sio wakati wake kwani bado watu wapo kwenye maombolezoo ya mtoto marerhemu Patrick.

”Hakutakiwa kusema chochote kwa kipindi hiki kabisa anatufanya sisi wanawake wengine tunadharaulika kama hatuna mapenzi, hatuna moyo, hatuna mapenzi na watoto, ni kweli angeongea lakini sio leo hiki ni kipindi cha kumwombea mtoto” amesema Shilole.

Ametoa ushauri kuwa angesubiri arobaini ipitie ndiyo mambo hayo yaongelewe, aidha amewalaumu waandishi wa habari kwa kukubali kufanya nae mazungumzo kwani muda wake wa kuongea ulikuwa bado.

 

Mohamed Salah aponda raha fukwe za Panama
Video: Haijapata kutokea, Tundu Lissu amvaa JPM

Comments

comments