Mauaji ya wanawake wazee (Vikongwe) kukatwa mapanga kwa imani za kishirikina yamepungua kwa zaidi ya asilimia 98 katika wilaya ya kahama mkoani Shinyanga kutoka 17 katika pindi cha mwaka 2016 hadi wawili kwa mwaka 2017 baada ya jeshi la polisi kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba la kuwabini na kuwakamata watu wanaojihusisha na mauaji hayo.

Wastani wa vikongwe saba wameuawa kwa kukatwa mapanga kwa kila mwaka tangu 2015 hadi 2017 kwa sababu mbalimbali ikiwemo kugombea mashamba na imani za kishirikina, kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wilayani Kahama, Mrakibu wa Polisi, George Bagyemu katika Kikao cha Tathimini ya Utendaji kazi wa jeshi hilo wilayani humo.

Mrakibu huyo wa Polisi, amesema kwa mwaka jana wanayo furaha ya kuutaarifu Umma kuwa hawakuwahi kupokea taarifa ya kuuawa kikongwe kutokana na mikakati na malengo waliyokuwa wakijiwekea, licha ya kufanikiwa kuzima viashiria kadhaa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu amelitaka jeshi hilo la polisi wa wilaya kuhakikisha wanadhibiti vya kutosha matukio yote ya uhalifu zikiwemo ajali za barabarani kwa lengo la kuwa na maisha salama.

Amesema, madereva wengi wamekuwa wakiendesha magari yao kwa mwendo kasi, na kusababisha kugonga watoto wengi, na kumkataka Kamanda wa Wilaya kuhakikisha matukio ya ajali katika wilaya yao inafikia sifuri, kwani kama waliweza kwenye matukio ya mapanga hilo nalo litawezekana.

China kujenga Chuo cha usafirishaji nchini
Kagera Sugar yaambulia sare nyumbani