Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christine Mndeme amesema Mkoa huo umekusanya zaidi ya shilingi 255 Bilioni za mapato yatokanayo na shughuli za madini katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia madarakani.

Mndeme ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya kwenye kongamano la kuangazia mafanikio yaliyopatikana Mkoani Shinyanga, ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christine Mndeme.

Amesema, makusanyo hayo, yanahusisha ada za leseni, mirabaha na ada za ukaguzi zinazokusanywa kupitia wizara ya Madini na kwamba Mkoa huo umetoa leseni mbalimbali za madini 827, katika kipindi hicho.

Hata hivyo, amesema vituo viwili vya ununuzi wa madini vimeanzishwa katika kipindi hicho cha miaka miwili, ikiwa ni moja ya mkakati wa kusogeza huduma za biashara ya madini karibu na maeneo ya wachimbaji wadogo.

Kocha Dar City atamba Ligi ya RBA
Taifa Stars inapaswa kuipigania Tanzania