Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa anasikitika kuona Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO, wanaagiza panga na vifungashio kutoka nje ya nchi.

Amesema hayo Jana Septemba 22, 2021 baada ya kufungua maonesho ya tatu ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), kitaifa yaliyofanyika katika kiwanja cha Umoja, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Aidha Makamu wa Rais ameiagiza wizara ya Viwanda na Biashara kufanya tathmini ya kweli kwenye Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), limefanikiwa au kushindwa kwa kiasi gani katika kuleta tija katika kutekeleza wa malengo ya kuanzishwa kwake kwa miaka 48 iliyopita.

Amesema katika tathmini hiyo watakwenda na mapendekezo ya mikakati mipya itakayopelekea Tanzania kuweza kukidhi mahitaji ya uchumi wa kati ya mashine ndogo,za kati,vipuri,bidhaa na huduma katika karne ya 21.

“Wiziri wa Viwanda na Biashara uhakikishe na isimamie utekelezaji wa zoezi hilo na unipatie mrejesho kupitia kwa Waziri Mkuu,” amesema Makamu wa Rais Mpango.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samweli Gamakwa amesema baadhi ya shughuli za uwekezaji zimekuwa zikifanywa na wajasiriamali bila  kuangalia athari za shughuli zao katika mazingira.

Mashabiki wa Arsenal waombwa kusubiri
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 23, 2021