Beki kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Valencia ya Hispania Shkodran Mustafi amekubali kujiunga na Arsenal ya England, japo mazungumzo kati ya viongozi wa klabu hizo mbili yakiwa bado yanaendelea.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekua sokoni kwa majuma kadhaa akisaka namna ya kuziba pengo lililoachwa wazi na Per Mertesacker ambaye aliumia goti wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens kati kati ya mwezi uliopita, na mwishoni mwa juma alimpoteza beki mwingine Gabriel Paulista baada ya kuumkia kifundo cha mguu akiwa katika mpambano dhidi ya Man City.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England, kimetoa taarifa za beki huyo kukubali kuelekea kaskazini mwa jijini London.

Mabeki wa pembeni Nacho Monreal pamoja na Mathieu Debuchy wameshindwa mtihani wa kucheza kama walinzi wa kati, jambo ambalo liliongeza msukumo wa Wenger kuharakisha mpango wa usajili wa Mustafi mwenye umri wa miaka 24.

Beki huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014, amewahi kucheza soka nchini England wakiwa na klabu ya Everton, lakini hakubahatika kupandishwa katika kikosi cha wakubwa kufuatia klabu ya Sampdoria ya nchini Italia kumsajili akiwa kijana mdogo na baadae alijiunga na Valencia CF miaka miwili iliyopita.

Naibu Waziri Mpina Atembelea Taasisi Za Muungano Kwa Upande Wa Zanzibar
Kapombe: Mungu Atanisaidia Nitaivaa Yanga