Beki wa klabu ya Arsenal Shkodran Mustafi hatochukuliwa hatua zozote za kinidhamu na chama cha soka nchini England (FA), kufuatia aina ya ushangiliaji aliouonyesha, baada ya kufunga bao la kwanza wakati wa mchezo wa ligi mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Cardiff City.

Beki huyo kutoka nchini Ujerumani alishangulia kwa kuonyesha alama Albanian Eagle ambayo inahusishwa na siasa za Ulaya ya mashariki, huku akimfuata Granit Xhaka ambaye alipiga mpira wa kona ambao aliumalizia kwa kichwa.

Mshambuliaji wa Liverpool Xherdan Shaqiri na Xhaka walitozwa faini na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kushangilia kwa kutumia alama hiyo wakati wa mchezo wa fainali za kombe la dunia kati ya Uswiz dhidi ya Serbia.

Mbali na kutozwa faini ya Pauni 8,090, Xhaka na Shaqiri walipewa onyo kali na shirikisho la soka duniani FIFA la kutakiwa kutorudia kuonyesha alama hiyo wanapokua katika majukumu yao ya soka.

Image result for FA will not take action with Mustafi after controversial celebrationXherdan Shaqiri na Xhaka

Chama cha soka nchini England (FA) kimefanya uchunguzi wa kina na kimeona hakuna sababu yoyote ya kumchukulia hatua Mustafi, kutokana na kitendo alichokifanya kutokuwa sehemu ya vitendo vya utovu wa nidhamu katika ligi ya nchini humo.

Alama la Albanian Eagle ilikua ikitumika wakati wa harakati za eneo la Kosovo lilipokua likidai uhuru wa kujitawala kutoka kwenye makucha Albania tangu mwaka 1990.

Xhaka na Shaqiri, wana asili ya Albania kufuatia wazazi wao kuzalia kwenye eneo la Kosovo, na walionyesha alama ya Albanian Eagle walikua wanadhihirisha uhalali wa kuendelea kudai haki ya kutaka Kosovo kujitawala.

Walizibinya Kende zangu na kunipiga mabuti- Bobi Wine
BREAKING: Rais Magufuli akizungumza na wananchi Ukerewe