Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amefunguka kufuatia sakata la  baadhi ya nyimbo za wasanii wa Bongo kufungiwa, amesema Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia shoo nje ya nchi.

Amesema kuwa endapo msanii atafanya kitendo hiko atakuwa amekiuka sheria na kanuni za nchi.

”Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kufanyia show nje ya nchi ” amesema Shonza

Aidha amewaasa wasanii nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ufanisi na uweledi mkubwa ili kutokiuka sheria na taratibu za nchi kwa lengo la kuendeleza na kukuza muziki na maadili ya Tanzania.

Amewataka wasanii waige mfano wa mwanamuziki Alikiba kwani amesema anaiwakilisha vyema nchi ya Tanzania kimataifa.

” kwa mfano Alikiba ni msanii mkubwa wa kimataifa anaiwakilisha nchi vyema, lakini haimbi nyimbo lugha chafu wala video ambazo hazina maadili” Ameongezea Shonza

Amesema kama wizara ya Sanaa inataka sanaa iende pamoja na ukuaji wa maadili ya nchi, amesisitiza wasanii kutoa burudani huku wakilinda tamaduni za nchi yao.

Shonza amefunguka hayo kufuatia sakata la baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva kufungiwa nyimbo zao kwa kukiuka kanuni na maadili, kufuatia Sakata hilo msanii Roma Mkatoliki alifungiwa kujihusiha na muziki kwa muda wa miezi sita kwa kutotii agizo la Naibu huyo.

Video: Serikali kufunga mitambo ya mionzi hospitali ya Ocean Road
Watu 40 wauawa, nyumba 1000 za chomwa moto