Naibu Waziri wa Sanaa, Michezo na Burudani, Juliana Shonza amefunguka na kuzungumzia wimbo mpya wa Diamond pamoja na Rayvany na kusema kuwa ameufurahia wimbo huo na kuwa wamejitahidi kimaadili na sio kama nyimbo zao nyingine.

Shonza amesema hayo wakati alipozungumza na Wasafi TV.

Wimbo wa Tetema ni moja ya nyimbo ambazo video zake hazijaleta utata kama ambavyo kundi hilo limekuwa likisumbuliwa mara baada ya kuachia nyimbo zao, kama ambavyo nyimbo yao ya Nyegezi ilivyozuiliwa kutokana na maudhui yake kukosa maadili lakini tumeona hata katika video ya wimbo aliomshirikisha Omario wa African Beauty ambao ulifanya Basata Kuingilia kati.

Aidha mara baada ya kuachiwa kwa video ya wimbo huo wa Tetema wadukuzi wa mambo wameripoti kuwa wimbo huo katika baadhi ya Scene zimeibwa katika wimbo mwingine wa hip pop kutoka nje ya nchi.

 

Wananchi na Viongozi wa CCM Ngara washiriki ujenzi wa Madarasa
Wananchi Njombe waipigia magoti Serikali, 'Tusaidieni Jamani'

Comments

comments