Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kudhamini mashindano ya michezo kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kutengeneza wachezaji bora watakaowakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akifunga mashindano ya Jimbo la Mbeya Vijijini yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Oran Njeza.

“Napenda kuelekeza shukrani zangu za dhati kwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Njeza kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kuibua vipaji vya mpira wa Miguu” amesema Shonza

Aidha, Shonza amesema kuwa amefurahishwa zaidi kwa kuona mashindano hayo yameshirikisha watoto wa kike wanaocheza mpira wa miguu.

 

Pia Naibu Waziri Shonza amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)kufanya ziara katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kuibua vipaji vya wachezaji watakaosaidia kuunda timu nzuri ya vijana chini ya miaka 17.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Oran Njezi amesema kuwa michezo ni chanzo cha ajira na ujenzi wa afya bora hivyo ni budi kuzingatiwa .

 

CCM yawataja wagombea Ubunge, Nyalandu apata…
Marekani yaivuta Korea Kaskazini mezani